Friday, 28 June 2013

SOMA HII KISHA UTAFAKARI MUSTAKABALI WA TAIFA HILI.JE TUTAFIKA?


BUNGE lime'fungwa' leo, lina idadi ya wabunge 356+1(mwanasheria mkuu wa serikali)
Kwa siku kila Mbunge analamba Tsh laki 2(seat allowance). Wamekaa bungeni siku 78. Ina maana 200,000/=@day times 78 days= 15,600,000/= kwa kila mbunge tu. Sasat hiyo 15,600,000 zidisha mara wabunge 357 unapata Tsh 5,564,200,000/=(kama sikosei).
Mshahara wa Mbunge si chini ya Milioni 7 kwa Mwezi,kwa Miezi miwili waliyokaa mjengoni wamevuna Tsh 4,984,000,000/= Grand Total(jumla kuu) ni Tsh 10,548,200,000/= bila kuweka marupu rupu mengine ya hapa na pale ndani ya bunge,kamati za bunge n.k.
Aisee...! Hivi rasimu ya katiba mpya si imetaja kupunguzwa kwa wabunge?! Nadhani hili linahusu. Ikibaki vile vile mimi mwaka 2015 nagombea ubunge kupitia Chadema,make kupitia chadema tu,ubunge nje nje!
Tuache masihara nchi ina matumizi kuliko inachoingiza,kwa nini mbunge posho isiwe elfu 50 kwa siku na mshahara ukawa kama Milion 2.5? Duh! Nchi ya kitu kidogo hii! Kingi wanakitumia wao!
Mihela hiyo jamaniiii... kwa raia wa kawaida huko Tanzania anaishi chini ya dola 2 kwa siku(TSH 3200)!
je hapa unasemaje ??

HII NDIO HUKUMU YA AKINADADA MNAOPENDA MAISHA YA MKATO


MTANZANIA MHITIMU WA CHUO MWAKA JANA (SAADAH) AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA YENYE THAMANI YA TSH.MIL 170

                                                 
                           

A BUSINESSWOMAN, SAADA KILONGO (26), APPEARED BEFORE THE KISUTU RESIDENT MAGISTRATE'S COURT IN DAR ES SALAAM YESTERDAY CHARGED WITH TRAFFICKING NARCOTIC DRUGS WORTH MORE THAN 170M/-.


BEFORE SENIOR RESIDENT MAGISTRATE NYIGULILA MWASEBO, THE ACCUSED WAS NOT ALLOWED TO ENTER ANY PLEA TO THE CHARGE. SHE WAS REMANDED UNTIL JULY 10, THIS YEAR, WHEN THE CASE WILL BE MENTIONED.


STATE ATTORNEY PETER MAUGO ALLEGED THAT ON JUNE 24, THIS YEAR, THE ACCUSED, A RESIDENT OF MBEZI BEACH RAINBOW WAS FOUND TRAFFICKING NARCOTIC SUBSTANCES NAMELY EPHEDRINE HCL AT JULIUS NYERERE INTERNATIONAL AIRPORT (JNIA). THE PROSECUTOR SAID THAT THE DRUGS WERE VALUED 170,481,000/ 


HAYA SASA HII NDIO HABARI YA MUJINI KAH!! MWENYEZ MUNGU ATUEPUSHE NA TAMAA NA MABALAA KAMA HAYA, SO SAD JAMAN NA AMEMALIZA CHUO LAST YEAR, IM SPEECHLESS!!!

HUYU NDIE PAA JOE MBUNIFU WA MAJENZEZA YA AJABU DUNIANI KUTOKA GHANA

HAYA NDIO MAAJABU YA RAISI MTOTO ALIPOMTEMBELEA OBAMA IKULU

ULIMWENGU NA MALIMWENGU!!!!!MTOTO WA MIAKA SABA ANAENDESHA GARI AKIWA AMEMBEBA DEREVA MLEVI CHAKARI

Polisi nchini Australia wamempata na hatia mwanamume mmoja kwa kosa la ulevi. 

Hata hivyo polisi waliposimamisha gari lake walishtushwa sana kupata gari la mwanamume huyo mlevi likiwa linaendeshwa na mtoto mwenye umri wa miaka saba. Polisi walilazimika kusimamisha gari hilo kwani lilikuwa likiendeshwa huku taa zake zikiwa zimezimwa saa tisa usiku. 

Polisi wamemchukulia hatua mwanaume huyo kwa kosa la kuendesha gari katika mazingira hatari akiwa mlevi. Hata hivyo mtoto huyo yuko na jamaa zake

BIBI YAKE OBAMA KUTUA DARESALAAM KUMUONA MJUKUU WAKE


SIKU CHACHE KABLA YA ZIARA YA RAIS WA MAREKANI KUJA NCHINI TANZANIA IMEFAHAMIKA KUWA BIBI YAKE NA RAIS ''OBAMA'' MAMA SARAH OBAMA ANATARAJIA KUJA NCHINI TANZANIA KUJA KUMSALIMIA MJUKUU WAKE HUYO.
AKIZUNGUMZA  JUZI KIJIJINI KWAKE ENEO LA KWEGERO HUKO KISUMU BIBI HUYO ALIEZALIWA MWAKA 1922 AMESEMA KUWA HAJISKII VIBAYA OBAMA KUTOITEMBELEA KENYA KWANI ANAJUA KUWA OBAMA NI RAIS WA TAIFA KUBWA DUNIANI,HIVYO ANAKUWA NA RATIBA AMBAYO INAZINGATIA MAMBO MENGI NA NI VIGUMU SANA KUIVUNJA.
 
BIBI HUYO AMEENDELEA KUSEMA KUWA ANAJISIKIA FURAHA KUONA MJUKUU WAKE HUYO KUJA TANZANIA KWANI HISTORIA INAONYESHA KUWA KABILA LA KIJALUO LINAMUINGILIANO MKUBWA KATI YA NCHI HIZI MBILI ZA TANZANIA NA KENYA HIVYO WAO WANAAMINI KUWA OBAMA AMEITEMBELEA NCHI YA NYUMBANI KWAO.

HIZI NDIZO WENYEWE WANAITA MATATU CULTURE ZA NAIROBI ZENYE KILA AINA YA UBUNIFU NA INTANETI YA BURE












BARACK OBAMA AWASILI SENEGAL IKIWA NI ZIARA YAKE YA KWANZA KATIKA ZIARA YAKE BARANI AFRIKA




Hi ni ziara ya pili ya Rais Obama Afrika
Rais Barack Obama amewasili Senegal katika ziara yake ya wiki moja barani Afrika na anatarajia kuzuru Afrika Kusini na Tanzania akilenga kustawisha demokrasia na masuala ya uchumi.
Hii ni ziara ya pili ya Obama barani Afrika tangu achaguliwe Rais mwaka 2008.
Hata hivyo ziara yake inatarajiwa kufifishwa na hali mbaya ya afya inayomkabili aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela. Ikulu ya white house imesema kuwa itategemea uamuzi wa familia ya Bwana Mandela iwapo Rais Obama anaweza kumtembelea hospitalini.
Katika mkutano wake wa leo na rais wa nchi hiyo, Mackey Sall, Rais Obama anatajiriwa kuipa heko Senegal kwa rekodi yake nzuri ya uthabiti ikizingatiwa iko kwenya kanda yenya misukosuko ya kisiasa.
Maafisa wa Marekani wanasema kuwa muhimu katika ziara ya Obama ni kustawisha demokarsia na nchi zote tatu anazotembelea ziko na demokasria thabiti.
Ni ziara ya pili ya Obama katika bara la Afrika tangu kuwa rais wa Marekani mwaka 2008

MAADHIMISHO YA MIAKA KUMI YA KIFO CHA MCHEZAJI MARC VIVIEN FOE YAZUA TAFRANI HUKO CAMEROUN


Tarehe 26 mwezi Juni mwaka 2013,ilitimia miaka kumi tangu kufariki kwa mchezaji wa Kimataifa wa Cameroun Marc Vivien Foe, aliye anguka uwanjani wakati wa mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FIFA la Mabara mwaka 2003 nchini Ufaransa.
Serikali ya Cameroon hata hivyo iliahirisha shughuli kubwa iliyoandaliwa kwa ajili ya kumbukumbu ya kifo chake, hatua ambayo imezua malalamiko ya wananchi wengi wanaodai kupuuzwa kwa mchezaji huyo.
Kifo cha Foe kiliamsha taharuki kubwa Duniani hasa kwa kuzingatia kilitokea kwenye michuano mikubwa na wakati ambapo Cameroun ilikuwa na mashabiki lukuki kutokana na ubora wa timu yao.
Amekuwa ni mtu mwenye kuenziwa kwa kiwango cha juu kuanzia FIFA hadi vilabu alivyovitumikia wakati wa uhai wake hususan timu za Olympic Lyon, West Ham United na Manchester City.
Serikali ya Cameroun ilipanga maadhimisho makubwa ya kumkumbuka Foe akitimiza miaka kumi kaburini hivi leo na maandalizi yote yalikwisha kamilika, lakini imeahirisha na kusogeza mbele hadi mwezi ujao kwa ajili ya kupisha Mkutano Mkuu wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika Magharibi na Afrika ya Kati ulioanza jumatatu wiki hii Jijini Yaunde.
Wananchi wa nchi hiyo wameghadhibishwa na kitendo hicho na baadhi yao wamenukuliwa wakisema kuwa Rais Paul Biya na Serikali yake wameshindwa kuonyesha heshima inayomstahili marehemu Foe.

Taarifa ya Serikali imesema kuwa Imeandaa shughuli hiyo kwa wiki nzima kuanzia Julai 20 hadi 27 itakayofanyika kwenye kituo kilichopewa jina la mchezaji huyo katika eneo la Nkomo-Okoui, Jijini Yaunde.
Marc Vivien Foe alikufa kutokana na mshituko wa moyo katika mchezo dhidi ya Colombia na kifo chake kimechukuliwa kama fundisho kwa wadau wa mpira wa miguu duniani kuhakiki afya za wachezaji na hasa vipimo vya moyo kila wakati.
Jambo hilo bado linasugua vichwa vya watafiti wa afya na bado hakuna majibu ya moja kwa moja ya kwa nini wachezaji wanakufa viwanjani kwa matatizo ya moyo ilhali wanapimwa afya zao ipasavyo. Wengi bado wanakumbuka mkasa uliompata mchezaji wa ligi kuu ya England Fabrice Muamba aliyezimia kwa siku kadhaa baada ya kuanguka uwanjani kutokana na matatizo ya moyo, Muamba alisalimika na amejiuzulu kucheza mpira kabisa licha ya umri wake mdogo wa miaka 23.
Rekodi zinaonyesha kuwa tangu mwaka 2003 wanasoka 38 wamekufa viwanjani kutokana na kutatizwa na moyo akiwemo Alen Pamic wa Croatia aliyekufa Ijumaa ya wiki iliyopita baada ya moyo wake kusimama ghafla.
Jamii ya wapenda soka duniani imeendelea kumkumbuka na kumuenzi Foe kwa matukio mbalimbali na mwezi Mei mwaka huu, Mchezaji wa Kimataifa wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang alishinda tuzo ya Marc Vivien Foe inayotolewa kwa mchezaji bora kutoka Afrika miongoni mwa ambao wanacheza ligi kuu ya Ufaransa.
Barabara jirani na ulipo uwanja alipofia Stade de Gerland mjini Lyon imepewa jina lake wakati mjini Lens huko huko Ufaransa Mtaa unaolekea uwanja mkubwa wa soka Stade Bollaert umebatizwa jina lake pia. Kadhalika kwenye uwanja wa City of Manchester umejengwa mnara mdogo kwa ajili ya kumbukumbu yake.
Kijana mmoja mjini Garoua nchini Cameroun ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa Simba huwa hafi bali anasinzia tu, akimaanisha kwamba Wacameroun bado wapo na kipenzi chao Marc Vivien Foe wanayeamini kuwa amesinzia tu

HII NDIO MAANA HALISI YA UPENDO WANAOONYESHA WANANCHI WA SOUTH AFRIKA KWA MANDELA



Mandela bado anaugua sana hospitalini
Mamia ya watu wanaendelea kukusanyika nje ya hospitali alikolazwa Nelson Mandela mjini Pretoria Afrika Kusini. Inaarifiwa Mandela bado yuko hali mahututi.
Wamekuwa wakimuimbia nyimbo na kumuombea nje ya hospitali. Wengine wamekusanyika katika iliyokuwa makaazi ya Mandela mtaani Soweto.
Watu wana wasiwasi kuhusu hali y mandela lakini pia wanataka kuonyesha wanavyojivunia kiongozi wao ambaye wanamuona kama baba wa taifa lao.
Mandela , rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini, anaugua maradhi ya Mapafu.
Mamia ya wananchi walikesha kwa maombi maombi nje ya makaazi ya zamani ya aliyekuwa rais wa taifa hilo Nelson mtaani Soweto.
Rais Jacob Zuma amesema kuwa afya ya shujaa huyo aliyepigana dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini humo inaendelea kuimarika.
Mandela aliye na umri wa miaka 94 amekuwa hospitalini akiuguwa ugonjwa wa maambukizi ya mapafu.
Awali mwanawe wa kike, Makaziwe alisema afya ya babake inaendelea kuwa njema.
Aidha Makaziwe amevikashifu vyombo vya habari kwa kukita kambi nje ya hospitali alikolazwa shujaa huyo akisema wanahabari wanapaswa kumheshimu babaake.
Rais Jacob Zuma alisema Alhamisi kuwa hali ya Mandela iliimarika lakini bado yuko hali mahututi.
"leo angalau yuko sawa kidogo kuliko nilivyomwacha jana usiku,'' alisema Rais Zuma baada ya kuongea na madakatari wanaomtibu Mandela.
Bwana Zuma alifutilia mbali safari yake ya Msumbiji ili kumtembelea Mandela hospitalini.
Wakati huohuo mwanawe Mandela Makaziwe alisema Mzee 'bado yupo' na kuwa anaweza kuhisi mtu akimgusa

HII INADHIHIRISHA NI JINSI GANI TULIVYO WATUMWA WA KIFIKRA.


Leo jioni wakati natoka katika shughuli zangu nilipita maeneo ya Mwenge pale stand ya mabasi nimekuta kweupe wale vijana wanao uza nguo kwa kupanga chini na kuzishika sikuwaona ...nikauliza nikaambiwa wamefukuzwa kwa ajili Oboma Anakuja...Mmhhh Kazi kweli kweli ...
Wakati bado nashangaa shangaa Mara likaja gari la Polisi na Wale mgambo wa jiji...Mara nikaona watu wanakimbia huku na kule ...Kushangaa kumbe wale wamachinga bado wapo ila wanauza kwa kujificha ficha kwenye vichochoro vya maduka..Sasa Kimbembe kikaanza wale wanamgambo wakawafuata huko huko na kuanza kuwapiga na kuwavunjia meza na viti vyao...Kwa kweli iliniuma sana kuona watanzania wenzetu wakifanyiwa hivyo ....Bado sijapata jibu ...siko zote mbona hawakufukuzwa ?? Huu Ugeni ndio imekuwa Nogwaaaaa....Na uhakika kuna ambao wanalisha na kutunza familia kwa kazi hizi za umachinga sasa watakula wapi kama hali ndio hiyo???

HAKI YAO KAMA RAIA HALALI WA TANZANIA IKO WAPI?KISA OBAMA TUWAFUKUZE!

KM
Ongeza kichwa

 
 Hawa ni baadhi ya omba omba jijini Dar es Salaam wakihamishwa maeneo yao
ya kazi ya kuomba.Kama unavyoona kwa picha hawako tayari kuhama kwa sababu hawana kazi ya kufanya zaidi ya kuomba wa wapita njia.Hivyo wanajua kabisa kitendo cha kuwaondoa katikati ya jiji ni kuwaua na njaa.Ok wavumilie Obama akimaliza ziara yake huenda serikali itawaruhusu tena kuendelea kuomba katikati yajiji