Tuesday, 25 June 2013


*WANASWA KWENYE BODABODA WAKIWA NA BASTOLA YENYE RISASI NJE YA BENKI YA POSTA DAR

 Askari kanzu (kulia) akiwa ameshika bastola aliyokutwa nayo mtu mmoja aliyekuwa amepakiwa katika pikipiki aina ya Boxer yenye namba za usaji T 961 CJW katika mtaa wa Makunganya jirani kabisa na benki ya Posta jijini Dar es Salaam leo mchana. Kutokana na kuongezeka kwa matukio ya ujambazi wa kutumia pikipiki na silaha, polisi wameimarisha ulinzi na hasa katika maeneo ya mabenki, ambapo leo wamebahatika kucheza karata yao ya kwanza na kuwanasa jama hao. Haikuweza kufahamika mara moja kuwa jamaa hao waliokutwa na silaha hiyo kuwa walikuwa wakiimiliki kihalali ama la, na sababu za kuwa eneo hilo mida hiyo ya mchana wakiwa na silaha hiyo.
 Watuhumiwa hao wakijaribu kuwasiliana na ndugu jamaa zao kutafita msaada, baada ya kunaswa.
Askari Kanzu, akiikagua silaha hiyo na kukuta ikiwa na risasi za kutosha......Picha kwa hisani ya Habari Mseto Blog

HOMA YA MAPAMBANO YA NGUMI KATI YA WASANII V/SWABUNGE KWENYE TAMASHA LA MATUMAINI YAZIDI KPAMBA MOTO

Tamasha la Usiku wa Matumaini limepamba moto, homa kali inapanda upande wa masumbwi kati ya mastaa katika ulingo wa siasa, dhidi ya wale wa Bongo Movie ambao wanatarajiwa kupanda ulingoni na kufumuana vilivyo Julai 7 (Sabasaba), mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


Inaeleweka kuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, atapanda ulingoni kufumuana na staa wa Bongo Movie, Vincent Kigosi ‘Ray’ katika pambano la raundi sita.
Zitto ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzania Bungeni, vilevile akiwa Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, ameshaongea mengi kuhusu nafasi yake ya kumchapa Ray ambaye naye amesema hawezi kupoteza pambano hilo.
Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee, ameapa kupiga ngumi adimu na kumchakaza staa wa filamu Tanzania, Jacqueline Wolper.
Vilevile, Mbunge wa Viti Maalum (Vijana), Mkoa wa Mara kwa tiketi ya CCM, Ester Bulaya, atakuwa na kazi moja tu siku hiyo ya kutoana ngeu na mtaalam wa kucheza na kamera, Aunt Ezekiel.
Kuhusu jinsi wanavyojianda, soma tambo zao kila mmoja kwenye boksi lake:
HALIMA MDEE
Inaonekana Wolper hajawahi kupigwa, hii ni mashine kubwa sana. Kifua changu ni chepesi sana kwa sasa kutokana na mazoezi ninayofanya. Nina uhakika ngumi yangu moja tu itampeleka chini na mchezo utaishia hapo, kwa hiyo madaktari wampime afya mapema, nisije kuua.
ZITTO KABWE
Nimetoka jeshini hivi karibuni na nimefuzu kwa alama nzuri sana, hili suala Ray inabidi aliangalie kwa umakini. Mimi ni bondia mzuri sana, nitamchapa na hatamaliza raundi ya pili. Nafanya mazoezi mazito, najitesa kwa ajili yake.
WOLPER
Nimetoka Afrika Kusini juzijuzi kwa ajili ya kujiandaa na pambano langu na mheshimiwa Mdee. Nimekuwa nikimtamani kwa muda mrefu, sasa arobaini yake itafika Julai 7 pale Uwanja wa Taifa. Nawaomba radhi wananchi wa Kawe kwa sababu nitauweka pembeni uheshimiwa wake halafu nitampiga mbunge wao.
ESTER BULAYA
Mimi ni mtu wa Mara na kila mtu anajua watu wa Mara tupoje kwenye upande wa mkono. Aunt Ezekiel ajipange kisawasawa kwa sababu nimejiandaa kumkalisha raundi ya kwanza. Nitamuonesha siku hiyo kuwa mbali na ubunge, mimi ni bondia kamili ninayeweza kupigana ngumi za kulipwa.
RAY
Sipendi Zitto aone mazoezi yangu, ataogopa. Vifaa ninavyotumia kujiandaa na pambano lake ni vizito tena adimu sana. Nataka ajue kwamba nitampiga. Ni mheshimiwa, namheshimu sana ila pale ulingoni itabidi nimchape.
AUNT EZEKIEL
Salaam kwa mheshimiwa Ester Bulaya, nataka ajue kuwa mimi ngumi zangu ni nzito sana. Nawaomba watu wa huduma ya kwanza waweke karibu ambulance wakati nitakapopanda ulingoni, ngumi yangu moja itampeleka sakafuni na hatanyanyuka. Hivi sasa nimejichimbia, nikiibuka nitakuwa tayari kwa ajili ya kutoa dozi

AJALI YA BASI YAUA MAWILI DODOMA

http://www.youtube.com/watch?v=cAMlzPmwrMY&feature=youtu.be

KACHANGA KAKUTWA KAKIWA KAMEKUFA BAADA YA KUTUPWA KISIMANI BAADA YAKUZALWA

Sources state they saw the little unlucky child later and when they came for his rescue he was already swollen and floating lifelessly on the surface of the the dim water. Some women don't deserve to be called mothers.
Tears poured from neighbours, especially a young woman who has been trying to give birth for four years to no avail, as the police came to fetch out the baby from the well.
After a quick search by the police the mother's blood and placenta was seen on the ground a couple of meter's away from the scene of the crime.
The main suspect is already on her heels as she was warned by her close friends that the police have been involved
Read more: x

HIVI NDIVYO MAREKANI WALIVYOTOA ONYO KALI KWA MSAFARA WA RAIS OBAMA NCHINI TANZANIA



Dar es Salaam. Licha ya ujumbe wa Rais wa Marekani, Barrack Obama kutarajiwa kufikia katika hoteli kubwa zenye hadhi wakati kiongozi huyo atakapowasili nchini Julai Mosi mwaka huu, Ikulu ya Marekani imetoa tahadhari ya vyakula ambavyo hawatakiwi kuvigusa wakiwa nchini ikiwa ni pamoja na kutumia maji ya bomba.Mbali na tahadhari hiyo, ziara hiyo ya Obama itakuwa na ulinzi mkubwa ambao pengine haujawahi kutokea katika historia ya viongozi wa nje wanaotembelea Tanzania kwani utahusisha idadi kubwa ya magari, ndege za kijeshi na meli kubwa ya kivita ambazo zitakuwa zikifanya doria karibu na pwani ya Tanzania.Tahadhari za matumizi ya chakula, maji na nyinginezo zimetolewa katika nchi zote tatu za Afrika ambazo Obama atatembelea, kila moja kwa jinsi Wamarekani hao wanavyoitathmini.Rais Obama atatembelea nchi za Tanzania, Senegal na Afrika Kusini.UlinziVyombo vya usalama vya Marekani vimejipanga kuhakikisha ziara ya kiongozi huyo haivurugwi kwa namna yoyote ile. Tayari ndege za jeshi zilizobeba magari ya akiba 56, yakiwemo 14 aina ya ‘Cadillac One’ maalumu kwa ajili ya kiongozi huyo, yamewasili katika nchi hizo tatu za Afrika atakazotembelea.Kwa mujibu wa gazeti la Washington Post la Marekani, ndege hizo pia zimebeba malori matatu ambayo yamesheheni karatasi maalumu za kuzuia risasi kupenya kwenye vioo, zitakazobandikwa kwenye madirisha ya hoteli ambazo Rais Obama na ujumbe wake watafikia.Kwa mujibu wa gazeti hilo, mamia ya mashushushu wa Marekani tayari wako katika nchi hizo. Meli maalumu za kubeba ndege za kivita, maarufu kwa jina la ‘amphibious ship,’ ikiwa na hospitali maalumu na yenye vifaa vyote itaweka nanga baharini, jirani na nchi atakayokuwa Rais Obama, tayari kukabiliana na dharura yoyote itakayotokea. Gazeti hilo liliandika kuwa ndege za kivita za Marekani zitakuwa zikipeana zamu kufanya doria kwa saa 24, katika anga la nchi ambayo Rais Obama atakuwepo, iwapo ndege za ‘adui’ zitakaribia eneo linaloitwa ‘anga ya rais.’ Kwa mujibu wa gazeti hilo, ziara ya Rais Obama aliyoifanya hivi karibuni katika nchi za Ujerumani na Ireland Kaskazini, japo kulikuwa na gharama kwa walinzi, lakini safari za nchi za Afrika zimeelezwa kuwa na gharama kubwa zaidi.TahadhariKwa mujibu wa taarifa ya maelekezo ya Ikulu ya Marekani, ambayo Mwananchi imepata nakala yake, watu watakaokuwa kwenye msafara wa Obama wametakiwa kutotumia kachumbari. Pia imewataka kutumia maji ya chupa zaidi.“Kutokana na mfumo wa maji uliopo, tunashauri watu wetu kutumia maji ya chupa zaidi kwa kunywa na hata kwa kupiga mswaki,” ilisema taarifa hiyo.Kwa kuelewa fika tatizo la ugonjwa wa malaria nchini, ujumbe wa Obama umeshauriwa kutumia dawa ya mbu ya kupaka na kupuliza inayoitwa Deet.Deet ni dawa maarufu huko Marekani na ikiwa katika aina tofauti ikiwamo ya kupaka na kupuliza na imekuwa ikitumiwa na jeshi la Marekani kwenye vita mbalimbali tangu miaka ya 1940 kabla ya kuanza kutumiwa na raia mwaka 1957.ATM nazo nomaPia watu watakaokuwa kwenye msafara wa Rais Obama wametakiwa kuhakikisha wanatumia mashine za kutolea fedha (ATM) zilizoko karibu na hoteli watakazofikia.“Kuna tatizo la uhalifu kwa hiyo siyo vizuri kutumia ATM ambazo ziko katika sehemu zisizo salama. Pia katika kipindi watakachokuwa Tanzania watu wanapaswa kutumia teksi ambazo zimeidhinishwa na hoteli.“Pia siyo vizuri kuacha kompyuta ya fedha kwenye vyumba mtakavyolala. Pia kina mama wanapaswa kuchukua tahadhari ya mabegi yao watakapokuwa wanapita mitaani,” ilitahadharisha taarifa hiyo.Marekani yatoa onyo kali kwa msafara wa Rais Obama D

HIVI NDIVYO VYOMBO VYA HABARI WALIVOJIPANGA NJE YA HOSPITALI ALIYOLAZWA NELSON MANDELA.AMBPO INASEMEKANA HALI YAKE NI TETE


DAWA YA DHRAU NDO HII.UKIJIFANYA MBABE KUNA WABAE ZAIDI YAKO.CHEKI HII


RAPA KEKO KUTOKA UGANDA ATAMANI KUFANYA KAZI NA MWANA FA MSIKILIZE HAPA