Thursday, 27 June 2013

OXFAM YAIHIMIZA KWA SERIKALI NA SEKTA BINAFSI KUWEKEZA KATIKA KUWAWEZESHA WAKULIMA WADOGO NA WA KATI KUPITIA KAMPENI YAKE YA GROW


IMG_7191
Mwanasheria –Mshauri Mwelekezi katika Masuala ya Haki za Ardhi – Emmanuel Massawe akifafanua jambo kwa wageni waalikwa wakati wa hafla ya kuwatangaza rasmi mabalozi wa OXFAM katika Kampeni ya GROW nchini itakayowezesha mfumo wa chakula kuwa wa haki na salama.
Na.Mo Blog Team
Taasisi isiyo ya kiserikali ya OXFAM kwa kupitia Kampeni yake ya GROW imewakutanisha pamoja masupa staa saba wa Tanzania wakiwemo Mbunge wa Kawe Mh. Halima Mdee pamoja na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mh. Shy-Rose Bhanji kufanyakazi pamoja na vikundi vya wanawake wajasiriamali na wazalishaji, kwa lengo la kuhakikisha hakuna mtanzania atakayeteseka kwa njaa wakati mbinu za kilimo zinaweza kufanikiwa.
Akizungumza wakati wa kuwatambulisha rasmi mabalozi wa OXFAM kupitia kampeni hiyo, mmoja wa mabalozi hao Bi. Khadija Mwanamboka amesema kilimo sio tu ni sekta endelevu nchini Tanzania bali pia ni Nyanja inayowezesha kupatikana kwa chakula kwa familia na akiba ya chakula kwa taifa kwa kuwa asilimia 80 ya wajasiriamali nchini ni wakulima.
Nchini Tanzania takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 60 ya wajasiriamali wanawake wanajihusisha na kilimo kikiwepo cha mbogamboga na matunda.
Aidha kampeni hiyo inakusudia kuendeleza na kukuza uzalishaji utakaoyafanya mazao hayo ya kilimo kuwa na bei muafaka kwa faida ya wakulima hao wa chini na wa kati.
IMG_7195
Naibu Mkurugenzi Mkazi OXFAM-Justin Morgan akziungumza na wageni waalikwa namna kampeni hiyo itakavyofanya kazi zake za uhamasishaji hapa nchini.
IMG_7224
Mabalozi wa OXFAM katika kampeni ya GROW wakati wa hafla hiyo.
IMG_7262
Khadija Mwanamboka – Mbunifu wa Mavazi akipozi na Tuzo yake mara baada ya kutangazwa rasmi.
IMG_7249
Shamim Mwasha Fashion Blogger.
IMG_7257
Dina Marious- Mtangazaji wa Redio.
IMG_7240
Jacob Stephen Muigizaji.
IMG_7244
Masoud Kipanya Mchora Katuni.
IMG_7280
Mabalozi wa OXFAM katika kampeni ya GROW katika picha ya pamoja na Naibu Mkurugenzi Mkazi OXFAM-Justin Morgan (wa pili kushoto).
IMG_7236
Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki

RAISIOBAMA AANZA ZIARA YAKE KATIKA NCHI BAADHI ZA AFRICA


ObamainSenegal
Rais Obama na First Lady Michelle Obama wakiwa na Rais wa Senegal, Macky Sall na First Lady wa Senegal Ikulu Dakar, SenegalRais Obama yupo barani Afrika kwa ziara ambayo itamfikisha nchini Senegal, Tanzania na Afrika Kusini.Ameongozana na mkewe Michelle na watoto wao. Hii ni mara ya pili kwa Rais Obama kutembelea Afrika na mara ya kwanza tangu alipochaguliwa kuongoza kwa muhula wa pili. Wakati wa muhula wake wa kwanza Rais Obama alitembelea nchi za Ghana na Misri.

TUJIFUNZE UPENDO KUPITA KISA HIKI



Chipanzee born in a Russian Zoo,
after being abandoned by its mother
was adopted by a dog of the Mastiffbreed and his four adorable puppies
that make more than happy life of
small chimpanzeme 

JIFUNZE KUWA MBUNIFU KWENYE MAZINGIRA YAKO KUPITIA MIFANO HII














INAKARIRIWA KUWA HII NDIO LISTI YA WATU MAARUFU WENYE USHAWISHI MKUBWA ZAID DUNIANI


Ndani ya mwaka mmoja wametengeneza mamilioni ya Dola, Wanapendwa zaidi na watu duniani, Na hawa ndio ma-celeb wenye nguvu na ushawishi zaidi duniani [top 10].


Katika orodha hii nafasi ya kwanza kabisa anashikilia mwanamama Oprah, na hii ni kutokana na nguvu yake kubwa katika Televisheni pamoja na mitandao ya kijamii, na pia anamiliki wa Cable Network kubwa kabisa ya Oprah, na kwenye rekodi inaonyesha kuwa kati ya mwezi June 2012 na June 2013 amejivunia kiasi cha dola milioni 77, sawa na shilingi 124,008,500,000 za kitanzania .
Katika nafasi ya pili anasimama, Lady Gaga ambaye ana nyota ya kupendwa na watu kutoka kona zote za dunia, akiwa anaongoza kufuatwa katika social networks hasa kutokana na muonekano wake wa kitofauti zaidi na Uwezo kimuziki, licha ya kuwa nnje ya stage kwa muda akiwa anapona uparesheni ya hips, ameweza kujivunia dola milioni 80, sawa na pesa za kitanzania, shilingi 128,840,000,000 katika kipindi cha mwaka jana mpaka mwaka huu. 









Katika nafasi ya tatu anasimama TV/Film Director/Producer maarufu Steven Spielberg ambaye yupo nafasi ya juu kabisa na anaheshimika katika fani hiyo akiwa ni mtu mzima mwenye umri wa miaka 59, Huyu kwa mwaka amejitengenezea dola milioni 100, sawa na shilingi 161,050,000,000 za kitanzania.

                       

Katika nafasi inayofuata anasiamama mwanadada Beyonce ambaye mafanikio yake yanafahamika kote, akiwa amejivunia dola milioni 53, sawa na shilingi 85,356,500,000 za kitanzania.
Pia kuna mkongwe Madonna katika nafasi ya tano, akiwa ametengeneza dola milioni 125, sawa na shilingi 201,312,500,000 za kitanzania. 

Nafasi ya sina inashikiliwa na Taylor Swift, dola milioni 55, sawa na shilingi za kibongo 88,577,500,000.
Nafasi inayofuata inakamatwa na Jon Bon Jovi, dola 79, sawa na shilingi za bongo 127,229,500,000.
Nafasi ya saba inashikiliwa na mwanamichezo wa Tennis, Roger Federer ambaye anashikilia dili nono na makampuni makubwa mbalimbali hasa yale yanayofanya biashara ya vifaa vya michezo, dola milioni 71, pesa za madafu 114,345,500,000.
Nafasi inayofuata inashikiliwa na mwanamuziki kinda, Justin Bieber, dola milioni 85, zinazolingana na pesa za kibongo 93,409,000,000.


Na katika nafasi ya 10 yupo mtangazaji mkali kabisa wa TV, Ellen DeGeneres, huyu akiwa na dola milioni 83 ndani ya mwaka mmoja, sawa na shilingi 85,356,500,000 za Tanzania.
#Vigezo vya Forbes katika orodha hii vimezingatia mapato waliyoingiza wasanii hawa kutoka mwezi Juni mwaka jana mpaka mwaka huu, na pia namba ya watu ambao wanawatazama na kuwafuatilia kwa karibu

HIINDIO KALI YA MWAKA


WATANZANIA WAISHIO MIKOANI WAPIGWA MARUFUKU KWENDA DAR WAKATI WA ZIARA YA RAIS OBAMA....!!

Thursday, June 27, 2013 | 12:09 PM

 
Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe amewashauri watu walioko mikoani kusitisha safari za kuja Dar es Salaam wakati wa ziara ya Rais wa Marekani, Barrack Obama kutokana na wingi wa wageni katika jiji hilo.
Ugeni huo pamoja na ule wa viongozi kumi na moja kutoka nchi mbalimbali duniani watakaohudhuria mkutano wa kimataifa wa Smart Partnership utakaofunguliwa kesho na Rais Jakaya Kikwete kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, umesababisha kuimarishwa kwa ulinzi katika maeneo mbalimbali hasa katika hoteli za kitalii ambazo zimeanza utaratibu wa upekuzi kwa wageni wake.

Akizungumza na katika mahojiano na Redio ya Clouds jana, Membe alisema jiji limefurika kwa wingi wa wageni.
“Hoteli na nyumba za wageni zimefurika wageni na magari mengi yamekodiwa. Kwa ujumla, huduma za kijamii zitakuwa shida,” alisema.
Rais Obama na mkewe Michelle watawasili nchini Jumatatu na tayari wapambe na maofisa usalama kutokana Marekani wameanza kuwasili. Mbali ya ujio huo, wake wa marais kutoka nchi 14 za Afrika watakaokutana na Laura Bush, mke wa Rais wa zamani wa Marekani, George Bush. Pia Michelle atahudhuria mkutano huo utakaofanyika Jumanne na Jumatano ijayo.


“Jiji la Dar es Salaam litakuwa na mambo mengi kwa hiyo wale wenye kuja kutaka kustarehe wafute safari zao,” alisema na kuongeza: “Kama kuna watu ambao hawapo Dar es Salaam na hawana sababu za kuja mjini waache tu mpaka wageni watakapoondoka kwa sababu jiji la litakuwa limejaa na baadhi ya barabara zitachukuliwa zitumike na wageni hao.”
Alisema katika kipindi cha siku tano zijazo, baadhi ya barabara za Jiji la Dar es Salaam zitakuwa na shughuli nyingi na nyingine zitalazimika kufungwa. Barabara itakayofungwa ni pamoja na ile ya Mwai Kibaki na ile ya Bagamoyo itakuwa na shughuli nyingi pia wakati Michelle atakapokwenda Jumba la Makumbusho, Jumanne ijayo.

Wasafiri wa mikoani
Wasafiri wa mikoani wataathirika zaidi Jumanne ijayo wakati Rais Obama atakapokwenda kutembelea mitambo ya kufua umeme ya Kampuni ya Symbion Ubungo.
Kituo hicho kipo Barabara ya Morogoro, ambayo ndiyo inayotumiwa na magari yanayoingia na kutoka mikoani.
Rais Obama atakwenda katika kituo hicho yapata saa 4.00 asubuhi na kwa kiasi kikubwa itaathiri magari ya usafirishaji wa mizigo na abiria yatakayokuwa yanatoka na kuingia Dar es Salaam kabla na wakati huo