Thursday, 4 July 2013
HII NDIO TANO BORA YA WACHEZAJI MATAJIRI ZAIDI DUNIANI
![]() |
David Beckham mwenye umri wa miaka 37 huyu ndie anaeongoza ameweka kibindoni hadi sasa Paund za Kiingereza 175 milioni.....!! |
![]() |
2.Lionel Messi Mchezaji wa Barcelona mwenye umri mdogo na mwenye kasi zaidi uwanjani huyu hadi sasa kutokana na matangazo na kazi ya mpira ameingiza kiasi cha paund za kiingereza 115.5 Milioni.... |
![]() |
3.Cristiano Ronaldo mchezaji wa Real Madrid ya Uhispania huyu kutokana na matangazo na mikataba mbalimbali hadi sasa ameingiza kiasi cha paund za kiingereza 112 milioni.. |
![]() |
4.Ricardo Kaka mchezaji wa Real Madrid ndio anashikilia nafasi hii kwa sasa kutokana na matangazo na biashara zake binafsi ameingiza hadi sasa paund za kiingereza 66.5 milioni |
HATIMAYE RAIS MORSI AONDOLEWA MADARAKANI
JESHI LA MISRI LAMUONDOA MADARAKANI RAISI MOHAMMED MORSI

jeshi nchini Misri limemuondoa madarakani Rais aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia nchini humo Mohamed Morsi na imemteuwa kiongozi wa muda wa nchi baada ya maandamano makubwa yanayoipinga serikali.
Akihutubia kwa njia ya televisheni jumatano jioni, mkuu wa jeshi,Abdul Fatah Khalil Al-Sisi alisema katiba ya Misri imesitishwa kwa muda na mkuu wa mahakama ya katiba ameteuliwa kuwa kiongozi wa muda nchini humo.
Sisi alitangaza kwamba jeshi linaangalia watu wa Misri kufuatana na maandamano makubwa ya upinzani yakidai kuwa Rais Mohamed Morsi ajiuzulu.
Kufuatia hotuba ya kwenye televisheni Bwana Morsi alitoa taarifa kupitia akaunti yake ya Twitter, akiita hatua ya jeshi ni “mapinduzi kamili”. Aliwasihi wa-misri wote kukataa hatua ya jeshi lakini pia aliwataka kuwa na amani.
Kiongozi mpya wa muda nchini Misri, Adli Mansour ana umri wa miaka 68 ni mkuu wa sheria katika mahakama ya juu ya katiba. Ataapishwa alhamisi.
Kama sehemu ya mwongozo mpya unaoungwa mkono na jeshi kwa nchi, sisi aliutaka uchaguzi wa urais na wabunge, jopo kutathmini katiba na kamati ya mashauriano kitaifa. Alisema mwongozo ulikubaliwa na makundi kadhaa ya kisiasa.
Pia aliwasihi watu wa Misri kuepukana na ghasia. Jeshi lilimpa Bwana Morsi saa 48 kutatua matatizo ya kisiasa au kuwepo hatari ya jeshi kuingilia kati.
Viongozi wa jeshi walisema wataweka “mwongozo” kama tofauti kati ya serikali ya ki-islam na wapinzani wake hawatamaliza matatizo yao ifikapo jumatano mchana ya tarehe tatu mwezi wa saba mwaka 2013. Tarehe hiyo ya mwisho ilipita muda wake bila ya hatua zozote kuonekana.
Bwana Morsi hakika alikataa wito wa kujiuzulu na aliapa kuendelea kubaki madarakani hata kama itamsababishia kifo chake. Pia alilalamika jeshi kutoa kitisho chake cha kuingilia kati katika matatizo ya kisiasa.
Baruti zilipaa angani kwenye umati wa watu wanaocheza na kupeperusha bendera katika uwanja wa tahriri Square mjini cairo, kiini cha ghasia za mwaka 2011 ambazo zilimuondoa Rais wa muda mrefu nchini Misri, Hosni Mubarak.
Katika wiki ilizopita maandamano yenye ghasia kati ya wafuasi na wapinzani wa bwana Morsi yameuwa takribani watu 40.
Jeshi la Misri limetangaza kuchukua madaraka ya nchi hiyo huku likitangaza kuwa si mapinduzi lakini Mohamed Morsi si rais tena wa Misri. Tayari Saudia Arabia imetuma salamu za pongezi kwa mkuu wa jeshi la nchi hiyo kwa kuchukua madaraka.
Hali ya rais Morsi ilikuwa ngumu pale wananchi wake walipoamua kuingia mitaani kumpinga siku chche zilizopita kwa maandamano baada ya kujitwalia madaraka mengi kiutawala kama mtangulizi wake
HII NI HATUA YA KUPONGEZWA KWA JB
NIMETOA MAISHA YANGU YOTE KWA CHAKULA- JB
MWIGIZAJI Nyota katiaka tasnia ya filamu Swahiliwood Jacob Stephen ‘JB’ amesema kuwa maisha yake yote ameyatoa kwa watu wenye shida ya chakula baada ya kuwa balozi wa Oxfam katika kampeni inayoitwa Grow akiongea na FC msanii huyo mwigizaji bora kwa mwaka 2012/ 2013 amesema kuwa ndoto yake ni kuwasaidia watoto wasio na chakula.
.
.
“Kwanza namshukru Mungu kwa kuchaguliwa kuwa Balozi wa Oxfam na kupewa kazi ambayo nimekuwa nikiifikiria siku zote jinsi gani naweza kuwasaidia wenye matatizo ya chakula hasa watoto, kuanzia sasa maisha yangu yote nimeyatoa kwenye chakula nitahakikisha hasa watoto wanapata chakula nikiwa kama balozi wa Oxfam,”anasema JB
JB ni mwigizaji pekee ambaye amechaguliwa kutoka kundi la wasanii wa filamu baada ya nafasi hiyo kuachwa na marehemu Steven Kanumba ambaye alikuwa Balozi wa Oxfam, kwa sasa inawezekana JB ndiyo kawa mrithi wake baada ya takribani mwaka mmoja, wadau kuhofia kukosekana mrithi wa marehamu Kanumba
WASANII WA BONGO MJIFUNZE KUWA WAJASIRIAMALI KUPITIA HII
ANGALIA HAPA SIMU ZA MKONONI ZENYE JINA LA CHAMILIONE
Msanii maalufu afrika mashariki na kati JOSEE CHAMILIONE anaetamba na wimbo wake wa BADILISHA Hivi karibuni alitakiwa kuongeza hoda ya simu za mkononi zinazomilikiwa na yeye baada yakuisha kabisa katika soko, simu hizo zinazokubalika sana uganda,zimekuwa zikimuingizia kipato kikubwa chamilione kila siku. ni simu alizozitengeneza kwa ajili ya watu wa hali ya chini na zenye line mbili.
Proj J akikabithiwa simu na jose chamilioni ikiwa kwenye box, kwa hapa tanzania ndio mtanzania pekee anaetumia simu hio ya CHAMILION,akiongea na mwandishi wetu Professor jay alisema alipewa vitu vingi vya thamani sana na chamilion alipokwenda kwenye tamasha lake la BADILISHA CONCERT kama i pad ya kisasa kabisa n,k.
WASANII WA TANZANIA JIFUNZENI KUPITIA WASANII WA UGANDA
FULSA ZIPO
Subscribe to:
Posts (Atom)