Wednesday, 26 June 2013

HIVI NDIVYO MFALME MSWATI WA PILI ALIPOWASILI DAR

b2ap3_thumbnail_01.jpg

Mfalme Mswati, akishuka kwenye ndege yake wakati alipowasili jijini Dar es Salaam leo.
b2ap3_thumbnail_1_20130626-180459_1.jpg
Wasaidizi wake wakiimba nyimbo za kikabila kabla ya Mfalme wao kushuka ndegeni, haikuweza kufahamika kuwa ilikuwa ni mila za kwao au walikuwa wakitambika ama nini kilikuwa kikiendelea.
b2ap3_thumbnail_02.jpg
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Mfalme Mswati wa (ii) wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam leo Mfalme Mswati wa ii, amewasili nchini kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 'Smat Patnership' unaotarajia kuanza Juni 28 mwaka huu.
b2ap3_thumbnail_04.jpg
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Mfalme Mswati ii, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam,  leo.
b2ap3_thumbnail_03.jpg



b2ap3_thumbnail_05.jpg
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Mfalme Mswati ii, mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo Juni 28, 2013 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa 'Smat Patnership', unaotarajia kuanza Juni 28. Kushoto ni mke wa Mfalme Mswati

HIZI NDIZO SIFA ZINAZOPELEKEA RAIS OBAMA KUJA TANZANIA

Licha ya kuwapo hali ya kutoridhika na hali halisi ya nchi, kiuchumi, kisiasa na kijamii kutoka kwa baadhi ya Watanzania, hali inaonekana tofauti kwa Marekani ambayo mtazamo wake wa masuala ya nchi za nje unawakilisha mtazamo wa mataifa mengi ya magharibi. 

 Ukitaka kumfahamu mtu, tazama aina ya watu wanaomzunguka. Msemo huu unaweza kutumika kuielezea Tanzania hasa baada ya kupata fursa ya kutembelewa na marais wawili wa taifa lenye nguvu zaidi duniani.
 

Mara ya kwanza, Tanzania ilitembelewa na Rais wa Marekani aliyekuwapo madarakani, Bill Clinton, Agosti 28 hadi 29, 2000.

Pia, nchi ikapata tena fursa ya kutembelewa na Rais George Bush mwanzoni mwa 2008 na sasa nchi imepata fursa tena ya kutembelewa na rais mwingine wa nchi hiyo, Barack Obama, ambaye atakuwa ameambatana tena na Bush, jambo ambalo ni la kihistoria kwa bara hili.

Licha ya kuwapo hali ya kutoridhika na hali halisi ya nchi, kiuchumi, kisiasa na kijamii kutoka kwa baadhi ya Watanzania, hali inaonekana tofauti kwa Marekani ambayo mtazamo wake wa masuala ya nchi za nje unawakilisha mtazamo wa mataifa mengi ya magharibi.

Akizungumzia sababu za ziara hiyo kwa njia ya Conference call kutoka Washington, Makamu wa Ushauri wa Masuala ya Ulinzi wa Ikulu ya Marekani, Gayle Smith alisema Obama anakwenda Tanzania kwa sababu nchi hiyo ni rafiki mkuu wa Marekani Afrika Mashariki. Alisema Afrika hususan Tanzania, ni moja ya masoko muhimu yanayoibukia ulimwenguni na Marekani lazima iongeze harakati zake barani humo

Read more: http://talkbongo.blogspot.com/2013/06/marekani-yataja-sifa-za-obama-kuja.html#ixzz2XL05tVIu

MBWA AKUTWA AKILA KICHWA CHA MTU


KULITOKEA kisa hiki ni katika eneo la Baharini  katika eneo la Eldoret Magharibi pale mwenye boma alipoamka na kumpata mbwa wake akila kichwa cha binadamu.
Bw Julius Kemboi alisema mbwa huyo alikuwa mlangoni mwake huku akila  kichwa hicho ambacho kilikuwa kimeanza kuoza.

Bw Kemboi aliongezea kuwa alikimbia katika kituo cha polisi kilicho karibu naye cha Baharini kuripoti tukio hilo na aliporudi na mafisa wa polisi kuona tukio hilo, kichwa hicho kilikuwa hakipo tena.

“Niliamua kwenda kuwaarifu polisi na tuliporudi nao ili wakichukue, hatukikipata
tena na sielewi kilikuwa kimeenda wapi,” alisema Bw Kemboi.

Alisema kuwa haelewi ikiwa kichwa hicho kilichukuliwa na mbwa tena hadi mahali
pengine walianza msako katika kichaka kilicho karibu na ambapo waliupata
mwili bila kichwa huku ukiwa umeliwa na mbwa sehemu kadha.

Mafisa hao wa polisi waliuchukua mwili huo na kuupeleka katika hifadhi ya maiti ya
hospitali kuu ya rufaa na mafunzo ya Moi mjini Eldoret.
Naibu wa afisa mkuu wa polisi katika eneo hilo Charles Mutua alisema kuwa polisi wameanzisha uchunguzi kuhusu tukio hilo.
Mwili huo ulikuwa wa mwanamme

MOHAMED DEWJI AWA MTANZANIA WA KWANZA KUTAMBULIKA NA JARIDA LA KIMATAIFA LA FORBES AFRIKA.

Mjasirimali mchapakazi na Mbunge Kijana nchini Tanzania, Mohammed Dewji (MO) ametajwa katika jarida la Kimataifa la mabilionea duniani katika Nyanja za biashara (Forbes Africa Magazine) kama mjasirimali mwenye umri mdogo mwenye mafanikio ya kuigwa hapa Afrika na duniani kwa ujumla taarifa la Jarida hilo limeeleza.

Kwa mujibu wa taarifa hizo toka kwa Jarida hilo la Forbes African Magazine linasema amekuwa Mtanzania wa Kwanza kupata kuhojiwa na (Forbes Magazine) mafaniko, changamoto na matatizo kadhaa kwenye uwanja wa biashara kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati.
Mo akihojiwa na Jarida hilo alisema toka kwenye masaa mia moja kwa wiki na kutengeneza faida ya Millioni 85 dola za kimarekani! Ni mafanikio makubwa katika biashara Afrika.
Anasema ni safari ya takribani miaka 12 ya ushindani wa kibiashara ndani ya mipaka ya Tanzania na Afrika kwa ujumla.

“Nani anaweza kufikiri kwamba tunaweza kubadilisha biashara yetu toka Millioni 30 za kimarekani hadi dola Billioni 1.1 ndani ya miaka 12 tu,’ alinukuliwa akisema

 zijue sifa chache za Gari atakalotembelea OBAMA hapa Tz




2.halilipuki hata uchome kwa kibireti 

1.halipati pancha


kwenye tanki la mafuta



3.inatumia muda wa dk.2 kwa km 10




4.haliingiliki kwa risasi



5.lina kitanda na sehemu ya kuhifadhia 



chakula na vinywaji