
Bw Julius Kemboi alisema mbwa huyo alikuwa mlangoni mwake huku akila kichwa hicho ambacho kilikuwa kimeanza kuoza.
Bw Kemboi aliongezea kuwa alikimbia katika kituo cha polisi kilicho karibu naye cha Baharini kuripoti tukio hilo na aliporudi na mafisa wa polisi kuona tukio hilo, kichwa hicho kilikuwa hakipo tena.
“Niliamua kwenda kuwaarifu polisi na tuliporudi nao ili wakichukue, hatukikipata
tena na sielewi kilikuwa kimeenda wapi,” alisema Bw Kemboi.
Alisema kuwa haelewi ikiwa kichwa hicho kilichukuliwa na mbwa tena hadi mahali
pengine walianza msako katika kichaka kilicho karibu na ambapo waliupata
mwili bila kichwa huku ukiwa umeliwa na mbwa sehemu kadha.
Mafisa hao wa polisi waliuchukua mwili huo na kuupeleka katika hifadhi ya maiti ya
hospitali kuu ya rufaa na mafunzo ya Moi mjini Eldoret.
Naibu wa afisa mkuu wa polisi katika eneo hilo Charles Mutua alisema kuwa polisi wameanzisha uchunguzi kuhusu tukio hilo.
Mwili huo ulikuwa wa mwanamme
Mwili huo ulikuwa wa mwanamme
No comments:
Post a Comment