Friday, 28 June 2013

BIBI YAKE OBAMA KUTUA DARESALAAM KUMUONA MJUKUU WAKE


SIKU CHACHE KABLA YA ZIARA YA RAIS WA MAREKANI KUJA NCHINI TANZANIA IMEFAHAMIKA KUWA BIBI YAKE NA RAIS ''OBAMA'' MAMA SARAH OBAMA ANATARAJIA KUJA NCHINI TANZANIA KUJA KUMSALIMIA MJUKUU WAKE HUYO.
AKIZUNGUMZA  JUZI KIJIJINI KWAKE ENEO LA KWEGERO HUKO KISUMU BIBI HUYO ALIEZALIWA MWAKA 1922 AMESEMA KUWA HAJISKII VIBAYA OBAMA KUTOITEMBELEA KENYA KWANI ANAJUA KUWA OBAMA NI RAIS WA TAIFA KUBWA DUNIANI,HIVYO ANAKUWA NA RATIBA AMBAYO INAZINGATIA MAMBO MENGI NA NI VIGUMU SANA KUIVUNJA.
 
BIBI HUYO AMEENDELEA KUSEMA KUWA ANAJISIKIA FURAHA KUONA MJUKUU WAKE HUYO KUJA TANZANIA KWANI HISTORIA INAONYESHA KUWA KABILA LA KIJALUO LINAMUINGILIANO MKUBWA KATI YA NCHI HIZI MBILI ZA TANZANIA NA KENYA HIVYO WAO WANAAMINI KUWA OBAMA AMEITEMBELEA NCHI YA NYUMBANI KWAO.

No comments:

Post a Comment