Friday, 28 June 2013

ULIMWENGU NA MALIMWENGU!!!!!MTOTO WA MIAKA SABA ANAENDESHA GARI AKIWA AMEMBEBA DEREVA MLEVI CHAKARI

Polisi nchini Australia wamempata na hatia mwanamume mmoja kwa kosa la ulevi. 

Hata hivyo polisi waliposimamisha gari lake walishtushwa sana kupata gari la mwanamume huyo mlevi likiwa linaendeshwa na mtoto mwenye umri wa miaka saba. Polisi walilazimika kusimamisha gari hilo kwani lilikuwa likiendeshwa huku taa zake zikiwa zimezimwa saa tisa usiku. 

Polisi wamemchukulia hatua mwanaume huyo kwa kosa la kuendesha gari katika mazingira hatari akiwa mlevi. Hata hivyo mtoto huyo yuko na jamaa zake

No comments:

Post a Comment